• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China waanza hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2015-03-03 17:58:22


    Mkutano wa tatu wa Baraza la 12 la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC umefunguliwa hapa Beijing. Mkutano huo pamoja na wa bunge la umma la China utafungua wiki mbili muhimu zaidi katika kalenda ya siasa ya China kwa mwaka huu, ambapo wajumbe 2,153 wa baraza hilo watajadili mada mbalimbali muhimu kuhusu maendeleo ya nchi.
    Katika ufunguzi wa mkutano huo, mwenyekiti wa kamati ya taifa ya CPPCC Bw. Yu Zhengsheng alitoa ripoti kuhusu kazi ya kamati ya kudumu ya CPPCC katika mwaka uliopita na kuahidi kuwa, baraza hilo litaongeza juhudi zaidi kusaidia kuhimiza mageuzi bila ya kujali shinikizo la kupungua kwa uchumi.
    Yu amesema "Kazi Nne Kuu" zilizotolewa na rais Xi Jinping zitakuwa kazi kuu za baraza hilo, ambalo ni chombo cha ngazi ya juu zaidi cha kutoa ushauri wa kisiasa nchini China. Kazi hizo ni pamoja na kujenga kikamilifu jamii yenye maisha bora, kufanya mageuzi kwa kina, kuhimiza utawala kwa kufuata sheria, na kuongoza chama cha kikomunisti cha China kwa nidhamu kali.
    Viongozi mbalimbali wa chama cha kikomunisti cha China na serikali wakiwemo rais Xi Jinping, waziri mkuu Li Keqiang, na Spika wa bunge la umma la China Zhang Dejiang, wamehudhuria ufunguzi wa mkutano huo.
    Mkutano huo unafanyika karibu kwa wakati mmoja na mkutano wa bunge la umma la China, ambao utafanyika kati ya tarehe 5 hadi 15 mwezi huu. Mikutano hiyo miwili ni mikutano muhimu zaidi ya mwaka nchini China, ambapo mipango ya maendeleo ya siasa na uchumi inajadiliwa huku sera muhimu zikitolewa.
    Akizungumzia umuhimu wa mwaka huu katika maendeleo ya China, Yu amesema, mwaka huu ni muhimu katika mageuzi ya kina na ya pande zote nchini China. Pia ni mwaka unaofungua utawala kwa kufuata sheria, na mwaka wa kuhitimisha mpango wa 12 wa maendeleo ya miaka mitano, hivyo amewataka washauri wa baraza hilo kuzingatia kutoa ushauri na mapendekezo kuhusu mageuzi na maendeleo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako