• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi tatu za Afrika Magharibi zatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kuongeza misaada ili kupambana na Ebola

    (GMT+08:00) 2015-03-04 11:21:37

    Mkutano wa kimataifa kuhusu hali ya Afrika Magharibi baada ya ugonjwa wa Ebola umefanyika jana huko Brussels, nchini Belgium. Kwenye mkutano huo nchi tatu za Afrika Magharibi zimetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kuongeza misaada ili kupambana na Ebola na kufufua uchumi.

    Mkutano huo ulioitishwa kwa mapendekezo ya pamoja ya Umoja wa Ulaya, Liberia, Sierra Leone, Guinea, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Magharibi na Umoja wa Mataifa, umehudhuriwa na zaidi ya wajumbe 500 wakiwemo marais wa Liberia, Sierra Leone, Guinea, Jamhuri ya Congo na waziri mkuu wa Togo. Kwenye mkutano huo walijadili uzoefu uliopatikana tangu kuzuka kwa Ebola, kazi muhimu za sasa na jinsi jumuiya kimataifa itakavyozisaidia nchi tatu zilizokumbwa na Ebola kurejea katika hali ya kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako