Soka ya Russia lazima iondoe virusi vya ubaguzi wa rangi kabla ya kombe la dunia la mwaka 2018. Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Russia Anatoly Vorobyov. Kiongozi huyo amekiri kwamba sio kila kitu kinakwenda kwa wepesi katika juhudi zao za kuondoa tabia za vitendo vya ubaguzi na kusisitiza kuwa taifa hilo wenyeweji wa kombe la dunia linaangaliwa kwa makini dhidi ya vitendo vyake hivyo. Rais wa FIFA Sep Blatter alieleza wasiwasi wake juu ya ubaguzi kufuatia utafiti wa vitendo vya ubaguzi nchini humo. Ripoti za Fare network na Sova Center zimeonesha kuwa zaidi ya kesi 200 za ubaguzi wa rangi zinahusu soka ya Russia katika misimu miwili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |