Ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A iliendelea tena usiku wa kuamkia jana kwa kushuhudiwa mchezo mmoja wa kukata na shoka. AS Roma walikuwa wenyeji wa vinara wa ligi hiyo Juventus katika dimba la Olympic na hadi mwisho wa mtanange huo matokeo yalikuwa sare ya 1-1. Juventus bado ipo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 58 wakati nafasi ya pili ikibaki kwa AS Roma.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |