• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kibarua cha kocha wa Azam chaota mbawa siku chache baada ya kutolewa kombe la Mabingwa Afrika

    (GMT+08:00) 2015-03-04 13:44:46

    Hatimaye Azam imemtimua kocha wake Mcameroon Joseph Omog siku chache tu baada ya kutolewa na El Merreikh ya Sudan kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika taarifa iliyotolewa na uongozi wa Azam haikusema sababu za klabu hiyo kumfungashia virago Omog ambaye katika miezi 14 aliyokuwa Chamazi aliwasaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza. Tetesi za kutaka kutimuliwa Omog zilianza baada ya timu hiyo kutolewa katika robo fainali ya Kombe la Mapinduzi na Mtibwa Sugar kwa penalti, lakini uongozi wa Azam ulikanusha taarifa hizo. Tangu wakati huo Azam imekuwa haina matokeo mazuri katika Ligi Kuu. Hata hivyo, ndoto ya Azam kutaka kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika ilivunjika Jumamosi iliyopita baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa El Merreikh hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2. Mbali ya Omog, Azam pia imevunja mkataba na kocha wake msaidizi Ibrahim Shikanda aliyewahi kuwa mchezaji wa kikosi hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako