• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge 39 wafukuzwa ubunge kutokana na kukiuka sheria au nidhamu

    (GMT+08:00) 2015-03-04 14:50:31

    Mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China unatarajiwa kufunguliwa kesho mjini Beijing. Mkutano huo pamoja na ule wa mwaka wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China ulioanza jana imefungua wiki mbili muhimu zaidi katika kalenda ya siasa ya China mwaka huu.

    Msemaji wa mkutano wa bunge la umma la kitaifa, ambalo ni chombo cha utungaji wa sheria cha juu zaidi nchini China Bibi Fu Ying amesema, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita wabunge 39 walifukuzwa ubunge kutokana na makosa ya kukiuka nidhamu au sheria, hali ambayo inaonesha kuongezeka kwa mapambano dhidi ya rushwa na kuimarika kwa usimamizi dhidi ya wabunge. Msemaji huyo amesisitiza kuwa ubunge sio tu ni wadhifa, bali pia ni jukumu na wajibu unaobeba matarajio ya wananchi.

    Fu Ying ameongeza kuwa China itakamilisha mfumo wa sheria kwa ajili ya kupambana na rushwa.

    Akizungumzia bajeti ya kijeshi ya serikali amesema kasi ya ongezeko la bejeti ya kijeshi imepungua kwa asilimia 10 mwaka huu, kasi ambayo ni ndogo zaidi katika miaka mitano iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako