Mikopo iliyotolewa na China imekuwa nguvu mpya ya kuchochea uchumi wa Latin Amerika unaodidimia, ambayo imezidi ile iliyotolewa na Benki ya Dunia na Benki ya maendeleo ya Amerika kwa kanda hiyo.
Ripoti mpya iliyotolewa na jumuiya moja ya washauri mabingwa iliyoko mjini Washington inasema, mikopo iliyotolewa na China kwa nchi za Latin Amerika iliongezeka kwa asilimia 70 na kufikia dola bilioni 22 za kimarekani mwaka 2014, ambayo mingi kati yao ilitangazwa na rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara katika kanda hiyo mwezi Julai mwaka jana.
Argentina, Brazil, Ecuador na Venezuela ambazo haziwezi kukopa fedha kwa urahisi kutoka mashirika ya kifedha ya kimataifa, zimekuwa nchi za Latin Amerika zilinufaika zaidi na mikopo ya China mwaka 2014.
Ripoti hiyo pia imesema nchi hizo zimependelea zaidi mikopo kutoa China kwa kuwa China imeepusha kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |