• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Real Madrid mambo mabaya, Barcelona yawa vinara wa La Liga

    (GMT+08:00) 2015-03-09 15:48:17

    Real Madrid imeshindwa kuchukua fursa ya kuongoza katika ligi ya La Liga nchini Hispania baada ya kunyukwa bao 1-0 na kilabu ya Athletic Bilbao katika uwanja wa San Mames. Mshambuliaji wa kilabu ya Athletic Aritz Aduriz mwenye umri wa miaka 30 aliiweka kilabu ya nyumbani kifua mbele kwa kufunga kichwa kizuri baada ya kupata krosi safi kutoka kwa Mikel Ricos. Real Madrid ilitawala mchezo baada ya kipindi cha pili lakini mkwaju wa Gareth Bale uligonga mwamba. Lakini Athletic Bilbao ilikaza kamba na kupata ushindi huo. Nayo Barcelona jana iliamua kunyesha mvua ya magoli kwa kuicharaza Rayo Vallecano mabao 6 – 1. Katika mechi hiyo Lionel Messi alishinda magoli matatu kwa mara ya 24 ambapo ushindi huo umeifanya Barcelona ipande na kuwa vinara wa ligi ya La Liga. Naye Luis Suarez amefunga mabao mawili katika mechi ambayo Barcelona hata hawakuwa na huruma. Mbali na Suarez na Messi kufunga katika mchabango huo, Pique naye alizidi kuingarisha Barc katika dakika ya 49. Kwa Rayo ilipata goli la kufutia machozi lililoingizwa na Bueno katika dakika ya 80.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako