• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Arsenal yaingia nusu fainali baada ya kuilaza 2-1Manchester United

    (GMT+08:00) 2015-03-10 14:07:59

    Danny Welbeck ameipaisha Arsenal na kuipeleka kwenye hatua ya nusu fainali katika ligi ya Uingereza na kuifanya klabu yake ya zamani Manchester United kukiona cha mtema kuni kwa kumuuza msimu wa majira ya joto mwaka jana. Welbeck aliwaonesha ubabe Manchester United kwamba yeye ni bora kwa kufunga goli katika dakika ya 61 na kuiondoa kifua mbele timu yake kwa jumla ya magoli 2-1, katika mchezo ambao ulikutanisha timu mbili zenye mafanikio makubwa na zenye upinzani mkali. Katika mechi hiyo United ilipata pigo kubwa baada ya Angel Di Maria kufurushwa uwanjani kwa kurambwa kadi mbili za njano. United ilimuuza Wellbeck kwa pauni milioni 16, huku kocha Louis van Gaal akisema mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza hakuwa na kiwango cha washambuliaji wa klabu yake. Nacho Monreal aliifanya Arsenal iongoze katika kipindi cha kwanza lakini Wayne Rooney alisawazisha kwa kichwa safi katika dakika ya 29.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako