Floyd Mayweather asema "ulimwengu utasita" Mei 2 atakapo pambana na Manny Pacquiao
(GMT+08:00) 2015-03-12 14:03:54
Floyd Mayweather amesema "ulimwengu utasita" siku atakayopambana na Manny Pacquiao Mei 2 huku wakikutana uso kwa uso kwa mara mwisho kabla ya kuanza kupimwa. Mayweather aliyeshinda mapambano yote 47, amemwambia Pacqiao katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana huko Lo Angeles kwamba bado hajawa tayari kuonja ladha ya kushindwa. Awali Pacqiao alisema kwamba atamdunda Mmarekani huyo kwajili ya manufaa ya yake na ya mchezo wa ngumi. Mpiganaji huyo Mfilipino ana rikodi ya kushinda mapambano 57, kutoka sare mara mbili na kushindwa mara 5. Pambano la Mei, ambalo limekuwa gumzo kubwa kwa mazungumzo ya makubaliano yanayofikiwa na kusitishwa kwa zaidi ya miaka sita, linatarajiwa kuingiza kiasi cha pauni milioni 162 sawa na dola 250.