• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfuko wa Njia ya Hariri wakaribisha wawekezaji wa China na nchi za nje

    (GMT+08:00) 2015-03-12 16:36:55
    Meneja wa kampuni ya Mfuko wa Njia ya Hariri Bibi Jin Qi amesema, Mfuko wa Njia ya Hariri unaolenga kutafuta fursa ya maendeleo na uwekezaji kwa muda mrefu, unatoa huduma kwa lengo la kutimiza kuunganishwa kwa nchi na sehemu husika zilizoko kwenye "Eneo la kiuchumi la Njia ya Hariri na Njia ya Hariri baharini ya Karne 21", na wawekezaji wa China pamoja na nchi za nje wanakaribishwa kujiunga na mfuko huo.

    Bibi Jin Qi amejulisha kuwa mfuko huo wenye dola za kimarekani bilioni 40 ulidhaminiwa kwa pamoja na hazina ya fedha za kigeni ya China, Shirika la Uwekezaji la China, Benki ya EXIM ya China na Benki ya Maendeleo ya China, na unapenda kushirikiana na taasisi za fedha na mifuko mbalimbali ya kikanda na kimataifa katika kuwekeza na kukusanya mitaji, ili kusaidia kwa pamoja maendeleo na ustawi wa kanda hiyo na hata dunia nzima.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako