Taarifa kutoka FIFA imesema Zimbabwe imepigwa marufuku kushiriki katika mechi za kufuzu kombe la dunia kwa mwaka 2018, baada ya kuwepo kwa taarifa za nchi hiyo kukataa kumlipa kocha wake wa zamani, Jose Claudinei Georgini. Shrikisho la soka FIFA limesema limechukua hatua hiyo baada ya taifa hilo kushindwa kumlipa kocha huyo na kuongezea kuwa shirikisho la soka Zimbabwe, ZIFA lilishindwa kulipa deni hilo mbali ya kwamba walipewa muda wa kutosha ili kufanya malipo hayo. Marufuku hiyo inakatiza fursa ya taifa hilo kufuzu katika fainali za kombe hilo nchini Urusi kabla ya kuanza harakati zake za kutaka kufuzu. Mechi za kufuzu kwa michuano hiyo barani Afrika zinatarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu huku droo ikifanywa mnamo mwezi Julai mjini St Petersburg. Zimbabwe haijawahi kufuzu katika mechi za kombe la dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |