• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumizi yasiofaa ya dawa yaleta athari mbaya kwa watoto

    (GMT+08:00) 2015-03-16 09:51:55

    P. Karibu msikilizaji katika kipindi cha Sauti ya Wanawake kinachokujia kila jumatatu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataia. Katika kipindi hiki tunazungumzia masuala mbalimbali yanayomhusu mwanamke katika jamii, lakini pia hatuwezi kumsahau mtoto, kwani Mama na mwana!

    C. Katika kipindi cha leo tutazungumzia matumizi yasiyofaa ya dawa za watoto. Unajua Pili mara nyingi mtoto anaweza kukwambia kichwa kinauma, basi unachukua panadol au asprin, unakata nusu au robo, kisha unampa. Binafsi unaona hakuna madhara yoyote, lakini kumbe sivyo. Wataalam nchini China wana hofu kuhusu matumizi yasiofaa ya dawa kwa watoto, na wanashauri wazazi kupata usaidizi wa madaktari ili kulinda watoto kutokana na hatari yoyote.

    P. Naibu katibu wa shirikisho la China la habari zinazohusu dawa Bw. Xu Shuxiang amesema, matumizi yasiofaa ya dawa na kutumia vipimo kupita kiasi ni makosa makubwa yanayofanywa na wazazi nchini China. Amesema wazazi wengi huwapa watoto wao dawa kutokana na uelewa wao ambao sio wa kitaalam, jambo ambalo linahatarisha maisha ya baadae ya watoto hao. Ripoti iliyotolewa na shirikisho hilo inaonyesha kwamba, asilimia 32 ya watoto nchini China hupewa dawa kutumia vipimo visivyofaa, na asilimia 12.9 ya watoto wataathirika vibaya kutokana na dawa hizo.

    C. Naibu katibu huyo alitolea mfano kijiji cha Shiqiaocun kilichoko mkoani Henan ambapo wazazi wana ufahamu mdogo kuhusu dawa wanazofaa kuwapa watoto na kwa kuwa wengi wao hawapendi ladha ya dawa hizo, kwani labda huenda ni chungu, basi wanaamua kuwapa dawa za watu wazima. Hata hivyo Xu amesema kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu matumizi mabaya ya dawa kwa watoto imesaidia kupunguza tatizo hilo, na ufuatiliaji wa vipimo vinavyofaa umeongezeka zaidi miaka ya hivi karibuni. Pamoja na hilo, bado tatizo la kutokuwa na maelezo bayana kwenye dawa za watoto linaendela kuwepo.

    P. Mamlaka ya dawa na chakula ya China inasema, karibu vitengo 3, 500 vya dawa vinatumiwa nchini China, na chini ya asilimia 60 ni za watoto, lakini maelezo yanatolewa kwa asilimia 10 tu. Daktari Ding Guofang ambaye ni mkuu wa kitengo cha watoto wachanga katika hospitali ya Xiehe mjini Beijing anasema:

    "Tukitumia antibiotic kupita kiasi, hazitaweza kufanya kazi tena, vijidudu vitakuwa sugu, kwa sababu microorganism zina uwezo wa kujihifadhi. Basi tukitumia tena antibiotic, hazitakuwa na ufanisi kama zinavyotarajiwa. Kabla ya kutumia dawa hizo, ni lazima tufuate msingi fulani, tukithibisha mtoto ana maambukizi ya vijidudu, basi tunapaswa kutumia antibiotic, ama sivyo ugongjwa unaweza kudumu kwa muda mrefu, ama hatapata nafuu. Lakini mtoto akiambukizwa virusi, tusitumie dawa hizo. Pamoja na kuangalia joto la mwili wa mtoto, pia tuangalie ni aina gani ya vijidudu"

    C. Huyo ni Dr. Ding Guofang. Naye Mkurugenzi wa ofisi ya dawa katika hospitali ya watoto wa Beijing Wang Xiaoling anasema, dawa nyingi hazina maelekezo ya vipimo kwa ajili ya watoto, na katika kesi nyingine, kutoa dawa kwa kutumia vipimo vya watu wazima kunaweza kusababisha kuzidisha kipimo zaidi ya kinachotakiwa. Pia amesema, watoto wachanga, hususan wale wanaozaliwa, wako kwenye hatari ya kudhurika kutokana na kupewa dawa bila kufuata vipimo sahihi kwa kuwa viungo vya miili yao bado vinaendelea kukua.

    P. Dr. Wang anasema, toka mwaka 2011 hadi 2013, aina 1,098 za dawa zilitumika katika kliniki za watoto wachanga kwenye hospitali 15, lakini kati ya dawa hizo, ni 45 tu zilikuwa maalum kwa ajili ya watoto wadogo. Sasa licha ya uhaba wa dawa za watoto, viwanda vya madawa vinahofu ya kuingia kwenye sekta hiyo kutokana na kuongezeka kwa gharama, mchakato wa kupata idhini, na athari nyingine zinazohusiana na uzalishaji wa dawa kwa ajili ya watoto wachanga na watoto. Mwaka 2014, Wizara ya Afya na Uzazi wa Mpango ya China ikishirikiana na idara nyingine tano ilitoa mwongozo wa kukabiliana na uhaba wa dawa za watoto. Mwongozo huo unasema kuwa China itarahisisha mchakato wa kutoa idhini, itainga mkono utafiti na majaribio ya dawa, na kutoa sera nzuri za bei ili kuunga mkono uendelezaji wa dawa maalum kwa ajili ya watoto.

    C. Msikilizaji, mwenzetu Mark Muli alipata fursa ya kuongea na Dokta Mutuma wa hospitali kuu ya Nairobi kuhusu athari ya kuwapa watoto dawa bila ya kuzingatia vipimo halisi. Hebu tumsikilize

    C. Naam msikilizaji, hususan Mama, natumaini umesikiliza kwa makini madhara ya kumpa mtoto dawa bila ya kuzingatia vipimo sahini. Na mpaka hapo ndio tumekamilisha kipindi hiki cha Sauti ya Wanawake kwa siku ya leo. Asante kwa kuwa pamoja nasi, na kwa heri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako