• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jose Mourinho ajitapa kuwa yeye ni kocha bora kuliko wengine wote

    (GMT+08:00) 2015-03-17 14:06:08
    Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema hakuna kocha yeyote aliyebaki kwenye Ligi Kuu England ambaye anafikia ubora wake na kujigamba kwamba kama watakuwepo basi ni wachache sana. Chelsea imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Paris Saint-Germain kwa mabao ya ugenini, lakini ipo kwenye nafasi nzuri ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England huku tayari ikiwa imenyakua taji la Kombe la Ligi. Amesema anafurahi sana pale kitu cha kwanza anapojilinganisha na wengine na kuona kuna pengo kubwa sana kati yake na wao, Ameendelea kujinasibu kwa kusema anawaona kama sio wapinzani wake, na kikubwa anachofanya ni kuwaheshimu tu. Amesema kwenye Ligi Kuu aliyetwaa ubingwa mara mbili au zaidi ni yeye na Wenger. Pia kocha aliyeshinda kila taji nchini Uingereza yakiwemo Ngao ya Jamii, Kombe la Ligi, Kombe la FA, Ligi Kuu sio wengi waliofanya hivyo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako