Louis Van Gaal asema Angel Dimaria ataendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho
(GMT+08:00) 2015-03-17 14:06:43
Kumekuwa na tetesi kuhusu winga wa Manchester United Angel Di Maria kuwa yupo mbioni kuihama timu yake hiyo kutokana na kuonekana kushuka kiwango kwa kipindi chote alichokuwa ndani ya klabu hiyo. Lakini kocha wake Louis Van Gaal ametoa msimamo wake akisema winga Angel Dimaria ataendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho licha ya kuonekana kushuka kiwango. Kiwango dhaifu alichokionesha katika mchezo dhidi ya Arsenal kwa kufungwa magoli 2-1 kwenye kombe la FA imesababisha kuleta uvumi mwingi dhidi ya mchezaji huyo. Angel Dimaria alisaini mkataba na Manchester United mwaka jana na hadi sasa hajafunga goli hata moja licha ya kusaidia magoli matatu katika mechi zake 10 za mwisho tokea Disemba mwaka jana.