• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serena Williams aingia katika 16 bora kwenye michuano ya Indian Wells

    (GMT+08:00) 2015-03-17 14:07:57
    Mchezaji namba moja duniani wa tenisi Serena Williams ameingia katika 16 bora kwenye michuano ya Indian Wells baada ya kupata ushindi mnono wa seti 6-2 6-0 dhidi ya Zarina Diyas wa Kazakhstan. Sasa atakutana na Mmarekani mwenziwe Sloane Stephens baada ya ushindi wa dakika 53 katika raundi ya tatu ya michuano ya wazi ya BNP Paribas. Serena ambaye alisusia michuano hiyo kwa miaka 14 baada ya kuzomewa na kushambuliwa kwa maneno mwaka 2001, amesema sasa anajisikia vizuri kucheza katika michuano ya California. Kwa upande wake Stephens alimshinda bingwa mara mbili Svetlana Kuznetsova kwa 7-6 (7-4) 1-6 6-4 na kuweza kukwea hadi 16 bora ambapo atakutana na Williams.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako