Sunderland yaajiri kocha mpya baada ya kumtimua Gus Poyet
(GMT+08:00) 2015-03-19 14:09:51
Siku moja baada ya kumtimua kocha wake Gus Poyet klabu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza, Sunderland imemuajiri Dick Advocaat kama mkufunzi mkuu wa timu hiyo hadi mwisho wa msimu. Mkufunzi huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi anachukua hatamu wakati ambao ''the Black Cats'' wapo ukingoni kushuka daraja. Mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Ellis Short amesema kocha huyo mpya anafahamu fika wajibu wake. Advocaat, mwenye umri wa miaka 67, anachukua nafasi ya Poyet, aliye timuliwa siku ya Jumatatu baada ya mazoezi na mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo Margaret Byrne. Hata hivyo kocha huyo mpya amesema kuwa Sunderland ni klabu kubwa ambayo anafahamu haitakuwa rahisi kuinusuru. Advocaat alikuwa hana kazi tangu ajiuzulu kama kocha wa Serbia mwezi Novemba. Kocha huyu kutoka Uholanzi anajivunia tajriba kubwa akiwa amewahi kuhudumu katika wadhifa huo akiwa Rangers, PSV Eindhoven na Zenit St Petersburg. Aidha Advoocat aliwahi kuifunza timu ya taifa ya, Ubejiji Korea Kusini, mbali na kutwaa mataji makuu ya ligi ya uholanzi , Scotland na Urusi.