Mashindano ya kuogelea ya Klabu Bingwa ya Tanzania Bara na Visiwani kuanza kesho
(GMT+08:00) 2015-03-19 14:19:34
Mashindano ya kuogelea ya Klabu Bingwa ya Tanzania Bara na Visiwani yanatarajiwa kuanza kesho Machi 20 na kumalizika Machi 21, katika Bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam kwa kushirikisha vilabu 15 vya Tanzania bara na Zanzibar. Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania TSA Noel kihunsi, amesema mashindano hayo yatashirikisha muogeleaji mmoja mmoja kuanzia miaka tisa mpaka 15 ambapo kwa upande wa makundi watashiriki kuanzia miaka tisa mpaka 10, 10-11,11-12,12-13,13-14 na 14-15 na 15 na kuendelea ambayo ni huru kwa mtu yeyote kushiriki. Kihunsi amesema, mashindano hayo yatashirikisha umbali mbalimbali kuanzia mita 50, 100, 200, 800 na kuendelea huku ikishirikisha mitindo minne ya kuogelea. Kihunsi amesema, mashindano hayo yatasaidia kuweza kupata timu itakayoweza kushiriki mashindano mengine mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.