• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gerrard aisaidia Liverpool kufungwa na Manchester United, badaye aomba radhi

    (GMT+08:00) 2015-03-23 14:02:38
    Nahodha wa kilabu ya Liverpool Steven Gerrard alipewa kadi nyekundu sekunde 38 tu baada ya kuingia katika kipindi cha pili ili kuchukua nafasi ya Adam Lalana aliyejeruhiwa. Kutolewa huko kuliisaidia Manchester United kuishinda Liverpool katika uwanja wa nyumbani wa Anfield. Gerrard aliingizwa baada ya Juan mata kuifungia Manchester United bao la kwanza ili kuimarisha safu ya kati iliyokuwa ikitawaliwa na manchester United. Lakini nahodha huyo alitolewa haraka sana baada ya kumkanyaga kizembe Ander Herrera na kurambwa kadi nyekundu swala lililoathiri mchezo mzima wa Liverpool. Baadaye Juan Mata aliongezea msumari wa moto kwenye donda kwa kutunduka bao la pili alilofunga vizuri na hivyo basi kuipatia ushindi manchester united, ambao kocha Lous van Gaal alikuwa akiutamani kwa hamu kubwa ili kendelea kujiimarisha katika msimamo wa ligi ya Uingereza. Hata hivyo Gerrad ambaye anatarajiwa kujiunga na LA Galaxy mwishoni mwa msimu ameomba radhi kufuatia kutolewa kwenye mchezo na kuwaangusha wachezaji wenzake. Kwa sasa Gerrad atakosa mechi tatu.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako