Mwana mieleka wa Mexico afariki duniakatika pambano nchini Mexico
(GMT+08:00) 2015-03-23 14:03:58
Mwana mieleka mmoja wa Mexico amefariki dunia baada ya kupigwa ngumi shingoni ndani ya ukumbi wa miereka. Pedro Aguayo Ramirez mwenye umri wa miaka 35 anayejulikana kama Hijo del Perro Aguayo alianguka na kupoteza fahamu katika ulingo ndani ya ukumbi wa miereka baada ya kupigwa teke na mpinzani wake Oscar Gutierrez anayejulikana kama Rey Mysterio junior, kulingana na kanda ya video ya pigano hilo ilillofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Tijuan. Pigano hilo liliendelea kwa dakika mbili kabla ya mashabiki na refa kugundua kuwa Aguayo alikuwa amepata jereha baya na hapohapo kuanza kumshughulikia. Afisa wa ofisi ya mashtaka ya Baja mjini California Raul Gutierez alisema alipelekwa katika hospitali ya jirani na kufariki. Naye mkurugenzi wa shirikisho la miereka la AAA Joaquin Roldan aliandika kwenye mtando wa twitter kwamba hana la kusema kufuatia tukio hilo la kushangaza na pia kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Aguayo.