• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" laungwa mkono na nchi karibu 60

    (GMT+08:00) 2015-03-23 20:03:07

    Waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi amesema, pendekezo lililotolewa na China kuhusu kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja"limeungwa mkono na nchi karibu 60.

    Bw. Wang amesema ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia hivi sasa, China imependekeza kujenga uhusiano wa kimataifa wa aina mpya ambao kiini chake ni kuwa na ushirikiano wa kunufaishana, na inataka wazo hilo lidhihirike kwenye sekta mbalimbali zikiwemo siasa, uchumi, usalama na utamaduni, na nyinginezo zinazohusika kwenye ushirikiano kati ya China na nchi za nje.

    Bw. Wang ameongeza kuwa China inakaribisha nchi mbalimbali, mashirika ya kimataifa, makampuni ya kimataifa, mashirika ya kifedha, na mashirika yasiyo ya kiserikali kujiunga kwenye utekelezaji wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako