• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa FA Greg Dyke atangaza mipango ya kuweka kikomo cha wachezaji wasiotokea Ulaya

    (GMT+08:00) 2015-03-24 14:06:36
    Mwenyekiti wa FA Greg Dyke ameionya Ligi kuu ya soka nchini Uingereza kuwa iko kwenye hatari ya kutowajali Waingereza, huku likitolewa pendekezo jipya la kuweka kiwango maalumu cha wachezaji wasiotokea Ulaya katika shirikisho hilo la Uingereza. Katika pendekezo hilo la hivi karibuni lilitolewa na kamati yake iliyoanzishwa mwaka 2013 ili kuboresha timu za Uingereza, FA pia imebainisha mipango yake ya kuimarisha sheria ya kukuza na kuendeleza vipaji vya nyumbani. Kamati pia imependekeza kufanyiwa marekebisho sheria za vibali vya kazi. Katika mapendekezo hayo yaliyotolewa na FA yanataka mchezaji asajiliwe na klabu yake kuanzia umri wa miaka 15 yaani chini ya miaka 18 aweze kufuzu kama mchezaji wa nyumbani. Idadi ya chini ya wachezaji wa nyumbani katika kikosi cha mwanzo cha wachezaji 25 katika klabu kiongezeke kutoka wanane hadi 12, wachezaji bora tu wasiotokea Ulaya ndio watapewa ruhusa ya kucheza Uingereza. Wakati huohuo straika wa zamani wa Arsenal John Hartson amesema FA inatakiwa iwe makini kuhusu kitendo chake cha kuanzisha sheria mpya kwani wachezaji wa nje wanaweza kuboresha wenzao wa Uingereza.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako