Kiungo wa kati wa ''The Flying Eagles'' Bernard Bulbwa ndiye aliyepachika bao hilo katika kipindi cha kwanza. Kufuatia ushindi huo Nigeria sasa wamewazidi wapinzani wao Misri kwa zaidi ya mataji matatu. Timu hiyo ya Nigeria inaungana na Senegal, Ghana na Mali kuiwakilisha Afrika katika kombe la dunia la vijana wasiozidi umri wa miaka 20. The Flying Eagles wamejumuishwa kwenye kundi E ambapo wanatarajiwa kujiunga na Brazil, Korea Kaskazini na Hungary. Mashindano hayo yataaanza Mei 30 na kukamilika Juni 20 huko New Zealand.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |