• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hafla ya kutoa tuzo kwa madaktari bora wa China wanaotoa huduma nchi za nje yafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2015-03-24 20:46:31

    Hafla ya kutoa tuzo kwa madaktari bora wa China wanaotoa huduma nchi za nje imefanyika leo hapa Beijing, na wahudumu 10 wa matibabu wa China wamepewa tuzo hiyo kwa mwaka huu. Shirika la Afya Duniani nalo limepewa "tuzo ya kuhimiza afya duniani".

    Madaktari hayo ni pamoja na Bw.Wang Zhi Hui kutoka idara ya afya ya jeshi la majini la China, Bw. Wang Zhenchang kutoka Hospitali ya Urafiki ya Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya cha Beijing, na wengine wanane.

    Waandaaji wa shughuli hii ambao ni Shirikisho la Urafiki wa Watu wa China na nchi za nje, Kamati ya Afya na Uzazi wa Mpango ya China, na idara ya ugavi ya Jeshi la Ukombozi la Umma la China wamesema, hafla hiyo inalenga kuonesha upendo walio nao madaktari wa China wa kukabiliana na taabu, kujitolea, na kutibu wagonjwa, na kuonesha taswira nzuri ya watu wa China ya kupenda amani na kuthamini maisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako