• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa Baraza la Boao la Asia la mwaka 2015 wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2015-03-26 18:25:09

    Mkutano wa mwaka wa Baraza la Boao la Asia la Mwaka 2015 utakaofanya siku nne umefunguliwa leo. Wajumbe 1700 kutoka nchi mbalimbali duniani watajadili kwa kina kuhusu mada kuu ya "Siku Mpya za Mbele za Asia: Kupiga hatua kwa Jamii yenye Hatma ya Pamoja ."

    Rais Xi Jinping wa China atatoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo Ambao unahudhuriwa na viongozi wa nchi mbalimbali wakiwemo rais Yoweri Museveni wa Uganda, rais Edgar Lungu wa Zambia. Idadi ya viongozi wanaohudhuria mkutano huo imezidi ya miaka iliyopita, ambayo inaonesha viongozi wa nchi mbalimbali wanatilia maani mkutano huo.

    Mada ya Ushirikiano wa kikanda itapewa umuhimu mkubwa kwenye mkutano huo ambao umeweka ajenda kuhusu Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB, Mkakati wa Eneo la Kiuchumi la Njia Hariri na Njia Hariri Baharini ya Karne ya 21 uliotolewa na China, na Jumuiya ya nchi za Asia Kusini Mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako