• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa vyombo vya habari vya nchi 17 wasaini Pendekezo la Njia ya Hariri

    (GMT+08:00) 2015-03-27 10:42:12

    Viongozi 21 wa vyombo vya habari vya nchi 17 wamesaini Pendekezo la Njia ya Hariri kwenye mkutano wa Baraza la Boao la Asia unaofanyika huko Hainan, China, wakiahidi kuhakikisha utaratibu wa mawasiliano kwa wakati, kuhimiza mawasiliano ya watu, kutimiza lengo la kunufaishana, na kuhimiza kuundwa kwa jumuiya ya ushirikiano wa vyombo vya habari katika ukanda wa kiuchumi wa njia ya Hariri na kando ya njia ya Hariri baharini ya karne ya 21 katika wakati unaofaa.

    Viongozi hao wameona ushirikiano na maendeleo kati ya vyombo vya habari kutoka nchi zenye tamaduni tofauti vitasaidia kuongeza maelewano na uaminifu kati ya watu wa nchi mbalimbali, na kuhimiza mawasiliano kati ya ustaarabu tofauti, na hivyo kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu. Akiwa mjumbe aliyewakilisha upande unaotoa Pendekezo la Njia ya Hariri, mkuu wa Radio China Kimataifa Bw. Wang Gengnian alisoma pendekezo hilo kwenye mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako