• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asisitiza China itashikilia sera ya ujirani mwema na mkakati wa kufanya ushirikiano wa kunufaishana

    (GMT+08:00) 2015-03-29 19:28:30

    Rais Xi Jinping wa China amesema China itashikilia sera ya ujirani mwema na mkakati wa kufanya ushirikiano wa kunufaishana.

    Rais Xi alisema hayo leo wakati alipokutana na wajumbe wa baraza la awamu ya 4 la kongamano la Asia huko Boao, mkoani Hainan, kusini mwa China.

    Rais Xi amesema China na nchi nyingine duniani zinahusiana katika hatma na mustakbali wa siku za baadaye. Alisema China itaendelea kufuata njia ya kujiendeleza kwa amani, kujitahidi kusukuma ujenzi wa aina mpya ya uhusiano wa kimataifa wenye msisitizo wa kushirikiana na kunufaishana.

    Amesisitiza kuwa China itashikilia kanuni ya kutofungamana na upande wowote, ikitarajia kujipatia msukumo mkubwa zaidi wa maendeleo kwa kupitia kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na nchi nyingine duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako