• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa mwandamizi wa Chama cha CPC cha China aapa kuzidisha uhusiano kati ya vyama vya kisiasa na Tanzania, Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2015-03-29 19:53:27

    Naibu mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China Bw. Wang Jiarui amesema, chama cha Kikomunisti cha China CPC kiko tayari kuzidisha uhusiano wa chama kwa chama na chama cha Mapinduzi cha Tanzania na kile cha Zanu-PF cha Zimbabwe.

    Bw. Wang alisema hayo alipokutana na rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mjini Arusha, Tanzania, wakati walipohudhuria kongamano la viongozi vijana kati ya Afrika na China.

    Rais Kikwete na rais Mugabe walitoa pongezi katika ufunguzi wa mkutano huo na kueleza matumaini kuwa vijana kutoka Afrika na China wataenzi na kuendeleza urafiki wa jadi kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako