• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukatili dhidi ya wanawake na watoto majumbani

    (GMT+08:00) 2015-03-30 08:45:11





    Vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinafanyika kila mahali duniani. Kule nchini Tanzania hali ya wanawake pia inazidi kuwa mbaya ndani ya nchi hiyo inayosifiwa kuwa ni nchi ya amani. Kwani kuna tukio moja la kusikitisha sana liliwahi kutokea katika kijiji cha Nyantira Tarime Mara. Akielezea mkasa uliomkuba binti yake Mama mzazi wa binti huyo Bibi Rwakatare alisema, binti yake alikatwa mguu na mume wake na sasa ana mguu kibuku, na sababu kuu ya ukatili huo ni kwamba bawana huyo alikuwa na kimada nje na kumuona mke wake wa ndoa kuwa hana maana yoyote hadi kufikia kumpiga na kumkata mguu wake.

    Kwa kweli hiki ni kisa ambacho kinahuzunisha kwani bwana huyo pia alijaribu kumkata mkono na mguu wake wa kushoto lakini bahati nzuri haukutoka isipokuwa mguu wa kulia tu ndio alioubukua kabisa. Binti anasema anatamani sana kurudi nyumbani kwa wazazi wake, ila tatizo ni kwamba kwa kuwa alilipiwa mahari na mume wake ambaye ndiye aliyemkata panga mguuni na kuutoa, hawezi kurudi kwao, wala mama yake hawezi kumkubalia arudi kwao, mpaka baba yake aje atoe ruhusa ya yeye kurudi nyumbani au abaki kwa mume muuaji avumilie mfumo dume. Ingawa mume wake amefungwa lakini tayari ameshampa mwenziwe ulemavu wa kudumu.

    Hiyo ni moja tu kati ya kesi nyingi sana zinazowakabili wanawake na watoto katika sehemu mbalimbali duniani. Kule nchini Kenya nako wanawake wengi pia wanasumbuliwa na ukatili majumbani. Lakini cha kustaajabisha baadhi ya wakati wanawake wanaokwenda kuripoti polisi, hatua yoyote haichukuliwi na polisi hao hivyo shirika la mawakili wanawake huwa linashirikiana na wanawake wahanga ili kuhakikisha haki inatendeka. Wakili wa shirika la wanawake mawakili FIDA Bibi Jacqueline Ingutiah anaeleza kuwa, mara nyingi huwa wanakwenda mahakamani kuangalia kesi zinavyoendelea na kama kweli haki inatendeka. Pia amesema wanawake sio lazima wavumilie pale wanapofanyiwa ukatili majumbani, lakini watumie polisi watumie shirika la mawakili wanawake, ama kuongea na watu wanaowaamini ili kutatua ukatili huu.

    Ingawa sheria zinakataza vitendo vya kuwapiga wanawake na kuwanyanyasa majumbani lakini bado kuna tatizo la mila ambazo zinaruhusu wanawake wapigwe kama watawakosea waume zao, lakini mila hizohizo hazioneshi adhabu yoyote ya kumpa mwanamume endapo atamkosea mke wake. Na hapa ndio tunasema mfume dume bado umeshamiri na kuendekezwa zaidi katika jamii nyingi.

    Na kama alivyosema wakili Jacqueline jambo muhimu ni kuhakikisha wanawake endapo watafanyiwa ukatili majumbani wanaripoti mara moja kwani hata mtaalam wa kisaikolojia wa kampuni ya utoaji ushauri wa kisaikolojia ya Chenhui Beijing Bw. Lei Ming alisema ukifumbia macho vitendo hivyo hususana unapokumbwa kwa mara ya kwanza ni sawa na kushirikiana kisiri na mwanamume afanyae ukatili nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako