• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Je wewe huwa unaoga mara ngapi kwa siku?

    (GMT+08:00) 2015-04-04 16:03:21





    Kumwelimisha mwanamke ni manufaa kwa jamii nzima. Katika kipindi cha leo tutazungumzia suala tofauti kidogo ambalo kusema kweli limetugusa mpaka ikabidi tulizungumze kwenye kipindi hiki cha Sauti ya Wanawake. Swali ni kwamba, Je, wewe unaoga mara ngapi kwa siku? Kila mtu ana desturi yake, kuna baadhi ya watu wanaoga hata mara 4 kwa siku, lakini pia, wako wale ambao kwa wiki wanaogamara moja au zaidi sana mara mbili.

    Kusema kweli hili jambo ni la kushangaza sana. Binafsi nachukulia kuoga kama sehemu moja kubwa ya maisha yangu. Hususan kama mwanamke, hauna budi kuoga japo mara mbili kwa siku, lakini cha ajabu ni kuwa, wanawake wanne kati ya watano wamekiri wazi kuwa hawaogi kila siku, na wengine wanadai kuwa wanaweza kukaa kwa siku tatu bila miili yao kukutana na maji. Sasa hayo yamo kwenye utafiti uliofanywa nchini Uingereza hivi karibuni kukagua ngozi za wanawake 2,021 wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 50.

    Utafiti huo pia umegundua kuwa, asilimia hamsini na saba ya wanawake wa Uingereza wanakiri kutumia karatasi laini zenye maji maji kujifuta mwilini kabla ya kulala. Asilimia themanini na tisa ya wanawake wanajitetea kuwa wangependa sana kusafisha miili yao lakini uchovu wa asubuhi na jioni ndio unawafanya wasioge. Mmiliki wa kampuni ya afya ya Flint+Flint, Maxine Flint anasema kwamba, wale wanaojitetea wanajidanganya, na kutooga hasa asubuhi haikubaliki kijamii, kwa watu wanaotuzunguka, na sio afya.

    Hapa nchini China, kuna desturi ya kijadi ambayo, wamama waliojifungua, hawawezi kuoga katika mwezi wa kwanza. Maoni hayo yanatokana na wasiwasi kuwa wamama hao wakioga, afya zao zitaharibiwa kutokana na baridi, kwani katika kipindi hiki maalum, wanakuwa ni wadhaifu kutokana na kujifungua. Hii ni tofauti kati ya desturi ya dunia ya magharibi na mashariki. Lakini hali inabadilika badilika hapa China, madaktari na wataalam hutoa pendekezo ambalo, si sahihi kujizuia kuoga baada ya kujifungua.

    Unajua binadamu tunatofautiana, lakini swali ni Je, unatakiwa kuoga mara ngapi? Jibu ni kuwa, sio mara nyingi kama wengi wanavyodhani. Unasikia? Madaktari wawili wa ngozi nchini Marekani wanasema kuwa, watu wengi wanaoga mara nyingi kuliko inavyotakiwa. Profesa Dr. Joshua Zeichner, wa kitengo cha ngozi katika hospitali ya Mount Sinai mjini New York Marekani anasema, kuoga mara nyingi, na kile tunachokiita harufu mbaya ya mwili ni hisia tu za kijamii. Mtazamo ambao Dr. Ranella Hirsch anakubaliana nao. Madaktari hao wanasema, kuoga mara nyingi unaweza kuleta madhara kwa mwili wa binadamu. Pia kunaweza kufanya ngozi iwe kavu na kusababishwa kuwashwa, ambako kutafanya ngozi ipasuke na kumweka mtu katika hatari ya kupata maambukizi. Lakini pia madaktari hao wanasema, wazazi hawatakiwi kuwaogesha watoto wao wachanga kila siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako