Habari kutoka Guinea ya Ikweta jana zinasema mkutano wa viongozi wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Kati CEEAC na jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi ECOWAS utaahirishwa hadi rais mpya wa Nigeria Bw. Muhammadu Buhari atakapoapishwa.
Mkutano huo ulipangwa kufanyika kesho mjini Malabo, ajenda yake ikiwa ni mapambana dhidi ya kundi lenye msimamo mkali la "Boko Haram".
Ofisa habari wa Guinea ya Ikweta amesema mkutano huo utafanyika haraka iwezekanavyo baada ya rais Buhari kuapishwa, lakini siku haijaamuliwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |