• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga watacheza na Etoile du Sahel ya Tunisia katika michuano ya kombe la afrika

    (GMT+08:00) 2015-04-07 14:07:02
    Hatimaye wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya vilabu ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga watacheza na Etoile du Sahel ya Tunisia katika raundi ya pili ya michuano hiyo.

    Yanga imefanikiwa kuwatoa Platinum FC licha ya kufungwa 1-0 katika mechi ya marudiano iliyochezwa mjini Bulawayo, nchini Zimbabwe. Hii inafuatia ushindi wa 5-1 ambao Yanga iliipata katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Tanzania.

    Sahel ya Tunisia,ambayo ina uzoefu wa kucheza michuano mikubwa Afrika, imepata nafasi ya kucheza na Yanga baada ya kutoka sare ya 1-1 na timu ya Benfica de Luanda. Katika mechi ya kwanza, Watunisia walishinda 1-0.

    Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub "Cannavaro"amesema wapo tayari kucheza na timu yoyote katika michuano hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako