• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaanzisha baraza la washauri la "Ukanda Mmoja Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2015-04-08 19:31:18

    Baraza la washauri la "Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri baharini ya Karne ya 21" inayojulikana kama "Ukanda Mmoja Njia Moja" limeanzishwa leo hapa Beijing. Baraza hilo litafanya utafiti na kutoa ushauri kwa serikali ya China na za nchi nyingine zilizopo katika "Ukanda Mmoja Njia Moja", na kuhimiza mawasiliano kuhusu sera za nchi hizo na kati ya watu wao.

    Baraza hilo linaundwa na taasisi 56 za China ikiwemo Idara ya mawasiliano na nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, kituo cha utafiti wa maendeleo katika Baraza la Serikali la China, Taasisi ya Sayansi za Jamii ya China, na chuo kikuu cha Fudan. Baraza hilo limefungua mlango wake kwa majopo ya washauri ya nchi zilizo na zisizo kwenye "Ukanda Mmoja Njia Moja" ili kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi za Asia, Ulaya na Afrika.

    Pia baraza hilo litajitahidi kuhimiza mawasiliano kati ya washauri wa China na wa nchi za nje ili watu wanaoishi kwenye "Ukanda Mmoja Njia Moja" waweze kuelewa kwa usahihi pendekezo hilo na kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya utekelezaji wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako