• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gabon yatajwa kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017

    (GMT+08:00) 2015-04-09 16:31:55

    Ratiba ya michuano ya kuwania kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika imetolewa jana na tayari sasa Dunia imejua nani kaibuka na ushindi kati yao. Taarifa iliyotolea jana April 8 2015 kutoka Cairo, Misri ni kwamba Shirikisho hilo la soka Afrika CAF limetangaza kuwa Gabon imechaguliwa kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017. Ghana, Algeria na Gabon zote ziliangusha karata ya bahati nasibu kwenye Shirikisho la Soka Afrika CAF ambapo kila moja ilijipa nafasi ya kushinda ili kuteuliwa kuandaa Michuano ya CAF mwaka 2017. Libya ndio nchi iliyokuwa iandae michuano hiyo lakini iliomba iondolewe kwenye nafasi hiyo kutokana na hali ya usalama kuwa sio nzuri. Shirikisho la soka Afrika CAF limeichagua Gabon ambayo ilikuwa ikigombea nafasi hiyo pamoja na Ghana pamoja na Algeria ambayo huenda imepoteza nafasi hiyo kutokana na hali ya usalama katika viwanja vyake baada ya tukio la kifo cha mchezaji wa Cameroon, Albert Ebosse mwaka 2014. Katika michuano hiyo Tanzania imepangwa kucheza kundi G pamoja na nchi za Nigeria, Misri na Chad.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako