• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ronaldo afunga goli lake la 300, Barcelona ikashinda mechi yake ya tisa mfulululizo

    (GMT+08:00) 2015-04-09 16:32:32
    Mchezaji bora wa dunia na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amefunga goli lake la 300 wakati Real Madrid walipoicharaza Rayo Vallecano na kuendelea kuwa nyuma ya vinara wa La Liga Barcelona kwa pointi nne. Ronaldo jana usiku aliweka rekodi hiyo katika msururu wa rekodi nyingi ambazo ameziweka akiwa anaichezea klabu hii ya Hispania. Ronaldo hadi sasa amefunga jumla ya mabao 48 katika michezo 42 ya michuano mbalimbali na anamzidi mpinzani wake Lionel Messi kwa mabao matatu kwenye ligi ya Hispania. Wakati huohuo katika kuhakikisha kwamba Barcelona wanaendelea kuwa viongozi wa La Liga jana ilimpa kichapo cha mbwa Almeria kwa kuwavurumushia mabao 4 – 0 bila huruma. Barcelona imeshinda mechi yake ya tisa mfulululizo na kuendelea kudhibiti mbio hizo za soka. Kama kawaida yake Messi alikuwa wa kwanza kuliona lango la Armelia na kuwafungulia njia akina Suarez na Bartra kuendeleza kipigo dhidi ya Armelia. Hivi sasa Barcelona ina pointi 74 huku ikifuatiwa na Real Madrid yenye pointi 70.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako