• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CAF yabadilisha sheria inayothibi umri wa mgombea wa viti vya kamati kuu

    (GMT+08:00) 2015-04-09 16:33:39
    Shirikisho la soka barani Afrika, CAF limeondoa vipengele vinavyodhibiti umri wa wagombea viti vya kamati kuu. Hatua hii imechukuliwa ili kumruhusu rais wa sasa Issa Hayatou kuwania awamu nyengine ya uongozi. Viongozi wote wa mashirikisho ya soka 54 ya bara la Afrika walikubali mapendekezo hayo ambayo yaliondoa kipengee hicho. Kipengee hicho kilikuwa kinamzuia mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 70 kushikilia wadhfa wowote katika shirikisho.Viongozi hao walitumia kisingizio cha uwiano wa kanuni zao na zile za shirikisho la soka duniani FIFA. Hayatou, 68, sasa atakuwa huru kuwania awamu nyengine mwishoni mwa mwaka 2017. Hayatou anatarajia kuwania kiti hicho cha urais ambapo itamruhusu kuongoza hadi atakapotimu miaka 75 mwaka 2021. Awali wapinzani wa kiongozi huyo wa CAF walidai kuwa alikuwa akibadilisha sheria kwa madhumuni ya kumnyima mpinzani wake uwezo wa kushindana naye. Aidha CAF ilipopitisha sheria ya kumtaka muaniaji kiti cha urais kuwa mwenyekiti wa kamati kuu washindani wengi waliona kama ni njama ya kuzuia upinzani wa utawala wake. Sheria hiyo haipo katika shirikisho kuu la FIFA. Raiya huyo wa Cameroon ameliongoza shirikisho la Soka Afrika tangu mwaka wa 1988. Aidha Hayatou pia ni naibu rais wa FIFA na ni mmoja kati ya viongozi waliotumikia kwa muda mrefu.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako