• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la China la ukanda wa njia ya hariri na njia ya hariri ya baharini ya karne 21 laendana na malengo ya Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2015-04-10 11:27:48

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson jana hapa Beijing alisema pendekezo la China la kujenga ukanda wa njia ya hariri na njia ya hariri ya baharini ya karne 21 linaendana sana na malengo ya Umoja wa Mataifa.

    Bw. Eliasson aliyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari na kusema juhudi za China katika kuhimiza uwekezaji wa miundo mbinu ni hatua halisi zinazohitajika kwa ajili ya malengo ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa. Ameongeza kuwa anatumai benki ya uwekezaji wa miundo mbinu ya Asia AIIB itaonesha umuhimu wake na kuyasaidia mashirika yaliyopo ya kifedha kama vile Benki ya Dunia.

    Habari nyingine zinasema, mkutano wa ngazi ya juu wa baraza la maendeleo endelevu ya ushirikiano wa Kusini na Kusini utakaofanyika leo huko Hongkong utafuatilia pendekezo la ujenzi wa ukanda wa njia ya hariri na njia ya hariri ya baharini ya karne 21. Mwenyekiti wa kamati ya Asia na Pasifiki ya kamati ya mwongozo ya maendeleo endelevu ya Kusini na Kusini amesema, pendekezo hilo linaendana sana na ajenda ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo baada ya mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako