Bao la kwanza lilitiwa kimyani na Sergio Aguerro lakini vijana wa Old Trafford walisawazisha kupitia Ashley Young .
Maruane Fellaini alifunga kichwa kizuri kilichoiweka Manchester United kifua mbele kabla ya kiungo wa kati Juan Mata kufunga bao zuri.
Chris Smalling naye pia alitikisa wavu kwa kupiga kichwa mufti kilichomwacha kipa wa City bila jibu kabla ya Aguero kufunga bao la kufutia machozi na la pili kwa upande wa City ambo kwa sasa wamepoteza mechi sita kati ya nane walizocheza.
Katika mechi ya mapema viongozi wa ligi Chelsea waliendelea na matokeo mazuri baada ya kuwachapa wenyeji wao QPR bao 1-0.
Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas ndiye aliyefunga bao hilo la pekee.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |