• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuimarisha ushirikiano katika nyanja nane na nchi zilizo njia ya hariri

    (GMT+08:00) 2015-04-13 18:48:17

    Hivi karibuni China imetoa waraka kuhusu malengo na mpango wa utekelezaji wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", ikimaanisha pendekezo hilo lililotolewa mwaka jana na rais Xi Jinping wa China liliingia kipindi cha utekelezaji.

    "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ni kifupi kwa Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri ya Baharini ya Karne 21. Kwa mujibu wa takiwmu, pendekezo hilo linahusu nchi zaidi ya 60 duniani zenye asilimia 62 ya idadi ya jumla ya watu duniani na GDP ya dola trilioni 21 za kimarekani kiasi ambacho kinachukua theluthi moja ya GDP ya jumla ya dunia. Mmoja kati ya watungaji wa waraka wa malengo na mpango wa utekelezaji wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ambaye ni mkurugenzi wa ofisi ya uongozi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" chini ya baraza la serikali la China Ou Xiaoli amesema China itaimarisha ushirikiano katika nyanja nane na nchi zilizo sehemu njia ya hariri ilipopita, zikiwemo kuunganisha miundo mbinu, kuimarisha ushirikiano wa nishati, mambo ya fedha, na utamaduni.

    "Katika upande wa kuunganisha miundo mbinu, kazi yetu ni kujenga njia tatu zinazounganisha China na bahari ya Baltic, ghuba ya Uajemi na bahari ya Hindi. Katika upande wa ushirikiano wa nishati, cha muhimu zaidi ni kuimarisha ushirikiano na Asia ya Kati, Asia ya Magharibi na Russia, na pia kupanua njia za kusafirisha nishati, kama vile maboma ya kusafirishia mafuta na gesi chini ya bahari. Hali kadhalika kuimarisha ushirkiano katika uchimbaji wa madini katika nchi za nje."

    Naibu mkurugenzi wa kituo cha mawasiliano ya kiuchumi cha China Zhang Xiaoqiang anaone kuwa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" litatoa nafasi kubwa ya maendeleo kwa nchi husika.

    "Ukanda Mmoja na Njia Moja inaunganisha ukanda wa kiuchumi wa Asia Mashariki na Ukanda wa Kiuchumi wa Ulaya na Marekani, na kuruhusu nchi husika kutumia uwezo wake vilivyo, kuendeleza ushirikiano kwa kina, vivyo hivyo ushoroba mrefu zaidi wa kiuchimi wenye uhai mkubwa zaidi na mustakbali mzuri zaidi utaumbika duniani."

    Kwa mujibu wa ratiba, kabla ya Oktoba mwaka huu, mipango ya mikoa na miji mbalimbali iliyohusika na "Ukanda Mmoja na Njia Moja" itaunganishwa na mpango wa taifa zima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako