• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mgogoro waibuka kuhusu usimamizi wa wanariadha Kenya

    (GMT+08:00) 2015-04-14 15:55:05

    Mkuu wa chama cha wanariadha wa kulipwa nchini Kenya Wilson Kipsang amepinga vikali mpango wa chama cha riadhanchini humo kutaka kuwasimamia wanariadha ambao meneja wao wamesimamishwa kwa muda wa miezi sita na chama hicho.

    Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama cha riadha cha Kenya Isaiah Kiplagat mameneja hao waliosimamishwa ni Federico Rosa wa Italia na Gerald Vandeveen wa Uholanzi wakituhumiwa kwa kuhusika na dawa za kuongeza nguvu.

    Amesema Kiplagat kuwa kwa sasa watafanya uchunguzi kwa miezi hiyo sita na endapo watapatikana na hatia watafungiwa.

    Uamuzi huo unatokana na kashfa ya wanariadha wa Kenya kutumia dawa za kuongeza nguvu.

    Kufikia sasa zaidi ya wanariadha 30 wa Kenya wamepatikana na hatia ya kutumia dawa hizi za kusisimua misuli akiwemo bingwa mara mbili wa Boston Marathon Rita Jeptoo ambaye amefungiwa mwa miaka miwili.

    Miongoni mwa wanariadha ambao Rosa anawakilisha ni bingwa wa dunia mbio za mita mia nane Eunice Sum, Asbel Kiprop na Vivian Cheruiyiot,

    Naye Vandaveen baadhi ya wakimbiaji anaowakilisha Kipsang na anayeshikilia rekodi ya dunia ya marathon Dennis Kimetto.

    Kiplagat ameeleza kwa kipindi cha miezi hiyo sita ni chama hicho kitawakilisha wanariadha kama maajenti wao.

    Lakini Kipsang ambaye pia ni bingwa wa Boston Marathon anasema hawatakubali kamwe kusimamiwa na chama hicho kwa sababu hawana imani nao kwa maswala ya fedha.

    Kipsang amesema ni makosa kwa chama cha riadha nchini Kenya kufungia maneja wao bila kuwajulisha na kuwa na ushahidi wanahusika na madawa ya kuongeza nguvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako