Nooij amesema kuwa soka ni mchezo usiotabirika, haswa ikizangiwa kwamba Tanzania imepangwa katika kundi gumu na timu za Nigeria, Misri na Chad katika michuano ya kuwania kucheza Fainali hizo, hivyo chochote kinaweza kutokea kwani kushinda au kufungwa ni sehemu ya mchezo .
Na katika kile kichaoonekana kutoziogopa timu hizo, amesema Stars pia itaonesha ushindani wa hali ya juu
Michuano ya Cosafa itakayofanyika nchini Afrika ya Kusini siku chache zijazo itakuwa ni sehemu ya maandalizi kwa Stars, kwa mujibu wa Nooij, ambaye anasema Stars itahitajika kutoa ushindani mkubwa.
Taifa Stars itakuwa na kibarua kigumu katika kugombea nafasi mbili kwa ajili kwenda kucheza fainali.
Stars imeshuka katika viwango vya FIFA vya mwezi April vilivyotolewa Alhamis kutoka nafasi ya 100 mpaka nafasi ya 107 na kushuka huko kuna maanisha Nooij atalazimika kufanya kazi ya ziada kupenya katika tundu la sindano.
Licha ya kushuka nafasi nne katika viwango vya FIFA, Nigeria, sasa ikiwa nafasi ya 45 ni miongoni mwa timu ngumu barani Afrika zikiwa na historia ya kufuzu kucheza kombe la Mataifa ya Afrika na hata la Dunia, sambamba na Misri, ambayo imepanda nafasi 7 katika viwango hivyo na kuwa nafasi ya 51.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |