• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kizaa zaa katika mechi za robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2015-04-16 14:07:25
    Pazia la robo fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya limefunguliwa jana ambapo Real Madrid imekutana na mahasimu wao Atletico Madrid kwenye uwanja wa Vicente Caldero, Hispania. Macho na masikio ya mashabiki yalikuwa upande wa mechi hii. Dakika 90 za mchezo zikakamilika kwa sare ya kutokufungana, 0-0. Beki wa Real Madrid, Marcelo kabla ya mechi hiyo aliwaomba mashabiki wasiwe na hofu kwa kuwa kikosi chao kilikuwa kiko sawa kabisa, lakini imeonekana wapinzani wao pia walijipanga kuhakikisha hawafanyi makosa kuipoteza mechi hiyo ngumu. Upande mwingine ilikuwa patashika kati ya vigogo wa Juventus na Monaco, dakika 90 zikakamilika pamoja na za nyongeza nyingine nne lakini Juventus walitoka kifua mbele kwa goli 1-0, ambapo Arturo Vidal alishinda goli hilo pekee kwa njia ya penalti. Kimbembe kingine katika mechi za jana uwanjani, Bayern Munich walikunjana na FC Porto huku matokeo yakionesha Bayern ilikabwa koo kisawasawa kwa kuchakazwa magoli 3-1 huku Paris SG wakishikana mashati na FC Barcelona ambao nao pia waliwaondoa wenzao uwanjani kwa machozi baada ya kuwabandika magoli 3-1.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako