• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji wa zamani wa NFL Aaron Hernandez amepatikana na hatia ya mauaji

    (GMT+08:00) 2015-04-16 14:07:57
    Mchezaji wa zamani wa NFL wa New England Patriots Aaron Hernandez amepatikana na hatia ya mauaji ya rafiki yake aliyekuwa pia mchezaji wa soka ya Marekani. Hernandez amehukumiwa kifungo cha maisha jela bila msamaha. Alikamatwa mwaka 2013 na kushitakiwa kwa kumuua Odin Lloyd, mchezaji aliyekuwa akitoka na dada wa mchumba wake Hernandez. Mwili wa Lloyd, ulipatikana ukiwa na majeraha sita ya risasi umbali wa chini ya maili kutoka nyumbani kwa Hernandez. Wakati huo Hernandez alikuwa na mkataba wa $40m. lakini ndani ya saa alilokamatwa Hernandez Patriots wakamfukuza mchezaji huyo, bila kuzingatia kuwa ni mchezaji bora. Katika hatua ya ufungaji, wakili wake mtetezi alisema alikuwepo wakati wa mauaji hayo, lakini ni wengine ndio waliomuuwa mchezaji huyo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako