• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyota wa Manchester United Wayne Rooney awatupia dongo Chelsea

    (GMT+08:00) 2015-04-17 14:19:25
    Nyota wa Manchester United, Wayne Rooney amewatupia dongo Chelsea kwamba sasa wanawaza kitu gani watawafanya kwenye mchezo ujao. Man United kwa sasa ipo kwenye kiwango bora ikishusha vipigo mfululizo tena dhidi ya timu ngumu kama Tottenham Hotspur, Liverpool na Manchester City na inaamini timu inayofuatia ni Chelsea. Miamba hiyo ya Old Trafford Jumapili wiki hii itasafiri hadi Stamford Bridge kuifuata Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu England na itasaka ushindi wake wa saba mfululizo. Rooney akigoma kuzungumzia nafasi ya timu yake kwenye mbio za ubingwa msimu huu, lakini alisema Chelsea yenye nafasi ya kuwa mabingwa itakumbana na shida siku hiyo. Chelsea inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi na nafasi ya pili inashikwa na Arsenal na nafasi ya tatu imeketi Man United.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako