• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Blatter afananishwa na Yesu, Mandela

    (GMT+08:00) 2015-04-17 14:19:58
    Sepp Blatter amefananishwa na Yesu, Mandela na Winston Churchill ambapo wajumbe 10 wa Concafaf wakimuunga mkono kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi Mei. Tangazo hilo limetolewa katika baraza la Shirikisho la Soka la Marekani Kaskazini na Kati na Caribbean (Concafaf ). Rais wa Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Dominican Osiris Guzman amemfananisha Mswisi huyo na watu mashuhuru katika Historia wakiwemo Moses, Abraham Lincoln na Martin Luther King. Rais wa Concafaf amesema wajumbe wanatuma salamu kwamba wataendelea kumuunga mkono Blatter. Blatter ni miongoni mwa wagombea wanne. Wengine ni mchezaji wa zamani wa Ureno Luis Figo, mkuu wa Shirikisho la Soka la Uholanzi Michael van Praag na Mwanamfalme wa Jordan Ali Bin Al Hussein, ambapo pamoja na Blatter wote walikuwepo kwenye hotuba ya baraza iliyotolewa jana. Nalo Shirikisho la Soka la Trinidad & Tobago limemsifu Blatter kama "Baba wa Soka". Wakuu wa mashirikisho ya soka ya Jamaica, Haiti, Turks & Caicos, Cuba, Panama, St Vincent & the Grenadines na Puerto Rico pia yameeleza kumuunga mkono Blatter anayegombea kwa mara ya tano tangu mwaka 1998. Kuna wajumbe 41 wa Concafaf na uchaguzi utafanyika huko Zurich Mei 30.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako