• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Baraza la soka nchini Sierrra Leone wavunjika kufuatia mgogoro

    (GMT+08:00) 2015-04-20 15:27:35
    Mgogoro wa soka nchini Sierra Leone ulipamba moto wikiendi baada ya Shirikisho la Soka kusubiri mkutano wa baraza kwa muda mrefu huko Makeni na kuvunjika saa chache tu baada ya kuanza. Mkutano huo lilipangwa kudumu kwa siku mbili, lakini ulivunjika baada ya kutoelewana juu ya nani awawakilishe baadhi ya wajumbe wa shirikisho hilo. Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Taifa Patrick Coker ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo alisema anauvunja mkutano huo kutokana na kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu katika SLFA unaohusisha uwasilishaji hususan wa eneo la magaharibi, makocha, waamuzi, na mashirikisho ya wakongwe. Kulikuwa na vurugu kabla ya mkutano huo wa mwaka kuanza wakati maofisa wa polisi kuwazuia baadhi ya wadau, wanaodai kuwa wajumbe halali kuingia kwenye ukumbi wa mkutano. Hata hivyo baadaye waliamuriwa na waziri wa michezo Paul Kamara ambaye alihutubia katika ufunguzi wa mkutano kuingia ukumbini. Kamati kuu iliahirisha mkutano huo Januari mwaka huu kuitokana na Ebola, lakini hatua hiyo haikuungwa mkono na wajumbe wengi ambao walipanga baraza lisilo la kawaida kupitia mkutano kwa njia ya simu Disemba mwaka jana, baada ya kukataliwa ruhusa na polisi kukutana kwasababu ya sheria ya dharura ya afya ya jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako