• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fainali kombe la FA ni AstonVilla na Arsenal

    (GMT+08:00) 2015-04-20 15:28:10
    Aston Villa imetinga fainali ya kombe la FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 baada ya Fabian Delph kufunga bao la pili na la ushindi dhidi ya Liverpool katika mechi ya nusu fainali. Ushindi huo umeiwacha Liverpool bila kitu msimu huu. Liverpool ilianza kuongoza kupitia mchezaji Phillipe Coutinho ambaye alivamia lango la Aston Villa kabla ya kucheka na wavu licha ya kukabwa na wachezaji wa Villa. Lakini Villa walisawazisha kupitia Christian Benteke aliyepata pasi kutoka kwa Delph. Delph baadaye alifunga bao la pili baada ya kuwapita walinzi wa Liverpool na hatimaye kutinga fainali ya kombe hilo ambapo watakwaana na Arsenal mnamo tarehe 30 ambayo siku ya jumamosi nayo iliicharaza Reading kwa mabao 2-1. Katika mechi hiyo Reading ilicheza kufa na kupona ili kushiriki katika mechi ya fanaili ya kombe la FA katika uwanja wa Wemble. Reading ilitoka nyuma na kusawazisha na kufanya mechi hiyo kuchezwa katika muda wa ziada. Vilvile walishindwa kutumia nafasi muhimu kuilaza Arsenal. Makosa ya kipa Adam Federic yaliipatia Arsenal ushindi huku mechi hiyo ikikamilika 2-1 kupitia mabao yaliyofungwa na mchezaji nyota wa Arsenal Alexei Sanchez.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako