• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga SC ya Tanzania na Etoile du Sahel ya Tunisia nguvu sawa

    (GMT+08:00) 2015-04-20 15:29:59
    Yanga SC imetoshana nguvu na Etoile du Sahel ya Tunisia kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika 16 bora iliyochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga ilianza kwa kuongoza bao la kwanza katika Dakika ya kwanza la Penati iliyopigwa na Nahodha wake Nadir Haroub Canavaro. Etoile iliendelea kushambulia ambapo timu zote zilienda mapumziko huku Yanga ikiwa inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Etoile. Katika dakika ya kwanza ya kipindi cha pili, Etoile iliweza kusawazisha bao hilo hivyo kuwapa Yanga wakati mgumu kutimiza ndoto ya kuibuka na ushindi katika mechi hiyo. Kipindi cha pili cha mchezo kilimalizika huku timu zote zikilala sare ya bao 1-1 ambapo mechi inatarajiwa kurudiwa wiki mbili zijazo nchini Tunisia na Yanga ikifanikiwa kuwaondoa Etoile du Sahel itasuburi kucheza mechi ya mtoano dhidi ya timu mojawapo zitakazotolewa katika 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CL).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako