• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi mbalimbali na kampuni za kimataifa zatarajia kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2015-04-20 16:23:44

    Mabalozi wa nchi mbalimbali nchini China na wajumbe wa kampuni za kimataifa zaidi ya 300 hivi karibuni walikutana hapa Beijing kusikiliza maelezo yaliyotolewa na wataalamu kuhusu pendekezo la kimkakati la kujenga "Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri" na "Njia ya Hariri Baharini ya Karne ya 21" inayojulikana kama "Ukanda Mmoja Njia Moja", ambapo walieleza matarajio yao ya kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na kampuni za China.

    Akijibu swali la mjumbe wa kampuni ya Mitsubishi ya Japan, katibu mkuu wa bodi ya taaluma ya Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Zhang Yansheng alisema kwa kushirikiana na serikali ya China na kampuni za China, kampuni za Japan na nchi nyingine zinaweza kufaidika katika "Ukanda Mmoja Njia Moja", na pia zinaweza kupanua zaidi soko la China.

    "Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, kampuni za Japan zilianza 'kutoka nje', na kufanya sarafu ya Japan iwe ya kimataifa na kampuni za Japan kuwekeza nchi za nje, maarifa hayo ambayo yametoa mfano kwa kampuni za China, na pia tumefanya utafiti juu ya njia za ushirikiano zilizofuata kampuni za japan katika sehemu tofauti. Ndiyo maana, sio tu nchi zilizo katika 'Ukanda Mmoja Njia Moja" zinaweza kupata fursa, bali pia kwa kufanya ushirikiano 'Ukanda Mmoja Njia Moja" itazipatia fursa kampuni za Japan na nchi za magharibi. Kuna ofisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Marekani ambayo ni kampuni bora 500 duniani aliwahi kuniuliza kwamba ni lini wachina wataichukulia kama kampuni ya China, kupitia kushiriki kwenye ujenzi wa 'Ukanda Mmoja Njia Moja", kampuni kama hizo zitachukuliwa kama ni sehemu muhimu ya mchakato huo."

    Kampuni za kimataifa zilizoshiriki katika mkutano huo pia zilieleza matarajio yao ya kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja Njia Moja". Mkurugenzi wa masuala ya serikali na maendeleo endelevu wa Kampuni ya Schneider China Pei Jinlin anasema,

    "Tunatarajia sana kushiriki katika mkutano huo, ambapo tutaweza kusikiliza maelezo kuhusu sera, na pia tutajulishwa jinsi serikali itakavyoelekeza kampuni za kimataifa kama ya kwetu kuratibu 'Ukanda Mmoja Njia Moja" ili kupata ukuaji wa biashara yetu."

    Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa China nchini Australia Bibi Li Cuiqi amesema ushirikiano wa kampuni za Australia na China utakuwa na mustakbali mzuri.

    "Naona kutakuwa na fursa nyingi, kwani kampuni za Australia zina nguvu katika sekta ya ujenzi wa miundo mbinu, mitaji na huduma za kifedha. Na makubaliano ya biashara huria kati ya Australia na China pia yatatoa fursa nyingi za ushirikiano kwa nchi hizo katika kilimo, fedha na maeneo mengine. Pia naona tunaweza kushirikiana na wenzi wetu wa ushirikiano wa China katika mchakato wa 'kutoka nje', na kutengeneza fursa mpya za ushirikiano katika 'Ukanda Mmoja Njia Moja'."

    Naye balozi wa Ireland nchini China Paul Kavanagh amesema "Ukanda Mmoja Njia Moja" ni pendekezo la uwazi, ambalo halilengi nchi fulani. Ireland ina nguvu katika huduma za fedha, teknolojia ya kilimo, upashanaji wa habari na mawasiliano ya simu, na inatarajia kampuni za China kuwekeza nchini Ireland.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako