• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa baraza la Umoja wa Mataifa asema "Ukanda mmoja na Njia moja" ni mfano wa kuigwa wa maendeleo ya kunufaishana

    (GMT+08:00) 2015-04-21 10:22:00

    Mwenyekiti wa baraza la Umoja wa Mataifa Bw. Sam Kutesa jana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa alisema, pendekezo la kujenga "Ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri na Njia ya hariri ya baharini ya karne ya 21" lililotolewa na China ni mfano wa kuigwa kwa jumuiya ya kimataifa katika kutimiza maendeleo ya kunufaishana.

    Bw. Kutesa amsema:

    "Mimi natoka nchi inayoendelea ya Afrika. Naona pendekezo la China linaendana na mkakati wa maendeleo wa karne 21 wa nchi za Afrika katika kuimarisha ushirikiano, kuongeza ujenzi wa miundo mbinu na kupanua biashara na nje. Pendekezo hilo linaonyesha kuwa, ustawi wa nchi moja unahusiana kwa karibu na maendeleo ya uchumi wa nchi nyingine."

    Bw. Kutesa pia ameipongeza China kwa kushirikiana na nchi zinazoendelea.

    "China kwa muda mrefu inaonesha umuhimu wake katika ushirikiano wa kusini na kusini kwa kutumia uwezo wake mkubwa wa kiuchumi. Naishukuru China kwa kuunga mkono nchi zinazoendelea, na kulinda mfumo wa amani na usalama wa kimataifa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako